Breaking

Tuesday, September 27, 2022

WAHIMA / BAHIMA


#KARIBU_UIJUE_HOME

WAHIMA/BAHIMA ni watu gani?

WAHIMA ni jamii ya Wafugaji wanaopatikana ukanda wote wa maziwa makuu Hasa ktk nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC, ambako wanapatikana katika Makabila ya Wanyambo, Wanyankore,Wahangaza, Wazinza, Waha, Wasubi, wahaya, warundi, wanyamulenge na Wanyarwanda.

Koo kubwa za WAHIMA katika jamii hizo Ni WAYANGO/WAHINDA, WASHAMBO, WAZIGABA, WAKIMBIRI, WACHABA, WASHINGO, WAGAHE, WAITIRA, WASIITA, nk
Inaaminika WAHIMA walianza kutawanyika toka Kusini Magharibi mwa Uganda Hasa eneo la NKORE na BUNYORO Kati ya miaka ya 1400 mpaka 1700 na kuhamia Kusini Hasa eneo la mkoa wa KAGERA, Mashariki ya Rwanda, Geita, Mwanza(Uzinza), Kigoma na Kusini mwa Burundi Hasa kutokana na kutafuta maeneo ya malisho na kilimo, baada ya kufika maeneo hayo walijiunga na jamii za wakulima wa maeneo hayo na kuanzisha TAWALA za Kitemi ambazo Machifu walitoka Jamii ya Wahima Mfano
1:KARAGWE, IHANGIRO(MULEBA), RUSUBI(Biharamulo), UKEREWE NA BUZINZA zilitawaliwa na Ukoo wa WAHINDA

2:HERU-Kasulu ilitawaliwa na Ukoo wa WAKIMBIRI

3:BUYUNGU -Wahinda
Nk
Tawala za Rwanda, Nkalinzi, Kiziba na Burundi hazikutawaliwa na wahima Ila wahima walihamia na kuishi maeneo hayo pia.

Kwetu TANZANIA Kutokana na kupungua kwa Malisho na idadi ya Mifugo wahima walianza kujihusisha na kilimo pia na kuoana sana na jamii za wakulima hivyo kuunda Makabila yasiyo na Tabaka Kama WAHAYA, WANYAMBO, WAHA, WASUBI, WAZINZA ambao kumjua mtu Kama Ni muhima mpaka ujue ukoo wake Tofauti kabisa na ANKOLE Uganda ambako Wahima wengi huoana wao kwa wao.

Wahima Wana Utajiri mkubwa wa Ng'ombe aina ya Ankole/INYAMBO na Hufanana sura na jirani zao Wafugaji wa kitutsi kitendo ambacho husababisha wengi wao kuitwa Watutsi .

No comments:

Post a Comment

Pages