Breaking

Thursday, July 6, 2023

*ABACHWEZI NI AKINA NANI?? SEHEMU YA PILI*


*ABACHWEZI NI AKINA NANI?? SEHEMU YA PILI*

Abachwezi INATOKANA na neno chwezi ambalo Kwa kijerumani ni neno SCHWARZ. Neno hili Kwa kijerumani linamaanisha "BLACK".

Kwahiyo Abachwezi/ abaswezi/ Abalangila /Abasamize ni watu weusi wenye nguvu za kiroho AMBAO walikuwa ni Wamisiri na pia walikuwa ni WABANTU.

Wamisiri walitoka Kusini na kuelekea kaskazini na kuanzisha utawala wa NAPATA,KUSH, ETHIOPIA pamoja na MISIRI(Kemet).

Wachwezi walitumia maeneo ya Bunyoro kulima Mtama Kwa maana maeneo hayo yalikuwa ni yenye rutuba na yenye kupendeza sana na LUGHA Yao ilikuwa ni Luchwezi LUGHA ambayo imezaa LUGHA za Makabila ya kibantu kwenye eneo la Maziwa MAKUU.

Kemet ilikumbwa na uvamizi wa Assyrian ( Parestina) mwaka 663 BC.HORDES ndiye aliyepewa Command ya kuongoza uvamizi huo na Mfalme wao Aliyeitwa CYMBASES na kuiteka Kemet.

Tawala zote hizo za NAPATA, KUSH ETHIOPIA pamoja na Kemet, zote zilivamiwa na kushambuliwa kutoka pande zote za ukanda wa PWANI,hivyo njia ya Wamisiri kukimbia ilikuwa ni kukimbilia Kusini, Lakini MAJESHI YA wavamizi yaliwafuata Hadi Etheopia,hivyo watu walikimbia Hadi Kusini mwa Sudan (Uganda). Kwa kipindi hicho Ethiopia ilikuwa na jeshi Imara sana na kuwazuia wavamizi. MAJESHI yaliyokwenda Hadi Etheopia yalijulikana Kwa jina la FISH EATERS.

KASOME: HERODOTUS BOOK II OF HISTORIES.

Kundi la pili la Bachwezi waliohama Toka kaskazini na kurudi Kusini, lilikuwa na watu wasiopungua 150,000, lilikuwa na Jeshi, Watabiri, Wana anga, Wajenzi, (Army, priests, astronomers, physicians, sages, sorcerers, technocrats, Masons and large section of nobilities). Kwahiyo iliwabidi washuke na kuelekea Kusini ili kuokoa maisha Yao na ufalme wa utawala wao.

The Bachwezi warriors wore the golden bracelets and the Bachwezi princesses were some of the most beautiful women mortals had ever seen on Earth.

Kwa urembo huo wa akina mama wa Bachwezi, Kuna msemo wa ABAGULUSI husema kuwa , Ensi ekakolwa Ruhanga, nebilungi byoona biba bya Ruhanga.

Lakini pia bachwezi hao hao,baadae walijipanga na kurudi kuwavamia hao wavamizi na kukimbilia kaskazini mwa Kemet (Middle kingdom), hao BACHWEZI waliporudi kaskazini,ndipo walipoanzisha Tena utawala wa Wamisiri na ulijulikana kama utawala wa kati(middle kingdom) na hapo walikwenda na Mungu wao Aliyeitwa MUNGU AMUN(AMON, EMMA). 

Mwanzo Wamisiri (Kemet/Wakamau) walikuwa na Re(Mungu Jua/KAZOBA) Na watawala waliitwa Wana wa Mungu yaani Wana wa Re,. Baada ya kuwepo Kwa Mungu AMUN/ AMON/ EMMA pamoja na Mungu RE, hapo wakaunganishwa na kuwa Mungu mmoja WA jina AMUN RE /AMON RE/ EMMANUEL.









No comments:

Post a Comment

Pages