Afrika inahitaji kiongozi atakaetumia ukali kutufikisha tunapostahiki Afrika haihitaji viongozi wabembelezaji na waombolezaji kwasasa bado hatujafikia huko
Ukisoma historia zote za mataifa makubwa zimeendelea kibabe zimeendelea kwa nguvu hakuna nchi hata mmoja imekuzwa kwa demokrasia demokrasia wamekuja kuadapt tu mwishoni marekani imeendelea kwa kutumikosha plantation watumwa weusi babu zetu,China imeendelea kibabe,Ufaransa, Russia,Cuba na kila nchi usidhani hizo nchi zilianzishwa tu na zikawa kubwa hapana zilianza na hatua kama tuliyokua sisi kwa sasa Kisha wakaja viongozi waliotumia ukali kunyosha mataifa na yakanyoka ndipo wakaja kuanza na demokrasia inakuaje sisi kwenye hatua yetu hii tumaanza kung'ang'ana na demokrasia wakati Kuna Mambo ya msingi ya kuyafanya kwanza huo utaratibu hauwezekani
Usipumbazwe na Sera zao za kusambaza demokrasia duniani kote wao hawajali demokrasia demokrasia wanatumia tu Kama kigezo cha kufanya maovu wanavyotaka duniani hapa na kuwazubaisha watu wasifanye wanalotakiwa kufanya instead wafocus kwenye Mambo yasiyo ya msingi ingekua wanasambaza demokrasia kwanini wasingemtoa madarakani Mobutu Seseseko wa Kongo aloechukua nchi kibabe na kufujisha nchi vibaya Sana ? Kwakua hakuwapunga wao na mifumo Yao ya kibepari kwanini hawakumtoa madarakani Blasie Compaoree aliemuua Thomas Sankara na anatawala kipindi kirefu kwa dhuluma? Kwakua aliwasikiliza walichotaka usidanganyike wanakuja kuleta demokrasia Afrika wao hawajali kuhusu demokrasia Wala siasa ya Afrika wanachojali Ni maslahi yao ukiwapigia magoti hata uuwe taifa zima hawatoongea kitu Ila ukikataa kuwapigia magoti hata ulishe taifa zima watakuita dikteta tu tuanze kutumia akili waafrika sasa tumechezewa sana tutaamka lini
Mimi binafsi siamini kwenye demokrasia kwasasa Afrika inahitaji viongozi wakali watakaoweza kusimamia mapinduzi ya kiuchumi kisiasa na kijamii(desturi) kuonyesha njia ya baadae
tujifunze kutoka kwenye historia
No comments:
Post a Comment