Breaking

Tuesday, September 27, 2022

ASILI YA KARAGWE KA NONO NA MAANA YA WANYAMBO





Baada ya Omukama Nono kufika Kaaro Karungi hasa KARAGWE(jina la sasa)kwa zamani Kaaro Karungi ILIKUWA ikiunganisha Karagwe na Nkore..

Nono aliweza kuteuliwa na Omuchwezi WAMARA kuwa Mwangalizi wa eneo hilo,na aliteuliwa kutoka katika kikosi cha jeshi maalumu la Omuchwezi WAMARA ili kuangalia himaya ya KARAGWE, hivyo alikuwa ukoo wa Abasiita,Nono ndiye Omukama wa kwanza kuitawa Karagwe,.

Kuja kwake karagwe kutoka Kitara(Bunyoro) alikuja na ng'ombe wengi yeye pamoja na kundi la watu aliokuja nao ndani ya Karagwe, hivyo palitafutwa mahala pa kuwaficha ng'ombe hao ambao kwa kipindi hicho,Mali ilikuwa ni Kumiliki ng'ombe, kwahiyo palikuwa na kilima ambacho kwa chini yake palikuwa na bonde(Omukivamo) ambalo lilikuwa na ukungu mwingi sana,na ILIKUWA vigumu kwa watu kuweza kuelekea bondeni huko.

Kwahiyo,walipaona mahali salama na pazuri kwa kuweza kuwaficha ng'ombe wao bila MTU mwingine kujua,na mahali hapo walipoficha ng'ombe wao wakapaita kwa jina la KARAGWE ikiwa na maana ya HAZINA,kuwa walificha ng'ombe na kuwahifadhi huko bondeni chini ya Kilima.

Ng'ombe hao walikuwa ni aina ya ENYAMBO ambao walikuwa ndio wengi na wachache walikuwa ng'ombe aina ya BUGONDO,ambao walikuwa wakipendwa sana na aliyekuwa Mke wa Omuchwezi WAMARA aliyeitwa NYABUGONDO,ng'ombe sina ya Bugondo ILIKUWA ni vigumu sana kuwafuga,lakini maana Mke wa WAMARA alitoa ng'ombe aina hiyo wachache na Enyambo kuwa wengi.

Kahiyo maana ya wanyambo wanatokana na kuwa wafugaji wa ng'ombe aina ya ENYAMBO,hivyo wakaamua kujiita wanyambo (Abanyambo)ikimaanisha kuwa ni watu wenye ng'ombe aina ya ENYAMBO na kuwa wafugaji maarufu wa ENYAMBO.

No comments:

Post a Comment

Pages