Breaking

Tuesday, September 27, 2022

RAIS WA ETHIOPIA, SAHLE-WORK ZEWDE


Rais wa Ethiopia, Sahle-Work Zewde aligoma kuungana na Viongozi wengine wa Afrika waliotakiwa kupanda basi la pamoja wakati wa mazishi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

“Nahitaji kiwango cha heshima sawasawa na wanavyopewa wengine” alisema Mwanamama huyo aliyelazimisha kupatiwa usafiri wa gari rasmi la ubalozi kwenda kutoa heshima za mwisho.

Sahle-Work Zewde ni mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Ethiopia ambaye ni rais wa Ethiopia tangu 2018, akiwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.

Huyu ndiye rais wa Ethiopia ambaye tena alionyesha hadhi yake ya kipeke Kimataifa kwa kusimamia anachokiamini.

Wengi wanafahamu historia ya Ethiopia kuwa ndio Taifa ambalo halijawahi kutawaliwa na wakoloni na iliwapinga na kuwashinda wakoloni wa Italia.

Ethiopia inaendelea kuonyesha uthabiti wa msimamo wake duniani. Imeendelea kuwa moja ya nchi zenye nguvu katika bara la Afrika licha ya changamoto tofauti.

No comments:

Post a Comment

Pages