Breaking

Saturday, October 7, 2023

FIKIRIA KWA MAKINI HILI


FIKIRIA KWA MAKINI HILI

Mwafrika Mweusi, mnyonge wa dunia, Ndiye pekee katika jamii ya wanadamu ambaye amevurugwa akili kufikiri kwamba mababu zake walimpa laana ambayo imemzuia Kufikia malengo na matamanio ya maisha.  Karibu kila balaa analokutana nalo duniani ni kosa la babu fulani... Ambaye lazima afungwe na kutupwa kwa moto wa Roho Mtakatifu katika jina la Yesu.

 Wazungu hawana mababu wa kutisha ambao wamefanya mambo ya kutisha. Ni babu mweusi tu.  Kwa miaka mingi, babu mweusi ametukanwa sana na Wakristo/waislamu wanatoa zaka, wanakesha usiku kucha, wanafunga na kuomba kumwangamiza babu wa Kiafrika kwa jina la Yesu.  Babu mweusi ni mbaya sana hata alilaani watoto wake mwenyewe.

 Mwafrica Baada ya kuwalaani mababu zake waliompa uhai, mtu mweusi anazurura duniani kote kama kobe asiye na Shimo.  Hana uti wa mgongo.  Utambulisho ni sifuri.  Hivyo hakuna jamii inayomheshimu.  Amezuiliwa nchini Malaysia, amefungwa huko Kambodia.  Amepigwa risasi kama mbwa katika mitaa ya Amerika. Mtu anayejichukia na kudharau mizizi yake hastahili heshima yoyote.

 Muheshimu Babu zako ni hatua ya kwanza katika kurudisha urithi wako wa kiroho unapoanza kurejesha kumbukumbu za mababu zako utaanza kujitambua wewe ni nani kuwa tukana Babu zako sawa na kujitukana wewe mwenyewe jamii zingine duniani zinakucheka KWA huo ujinga wako wa kudharau mizimu yako..

Mababu wawe nawe🙏

No comments:

Post a Comment

Pages