Breaking

Saturday, October 7, 2023

"Lakini ni nini kilitokea wakati wakoloni walipo fanikiwa kutubadilisha waafrika na kutufanya waislamu na wakristo?

THE SONG IS OUT NOW MAMA AFRIKA 
"Lakini ni nini kilitokea wakati wakoloni walipo fanikiwa kutubadilisha waafrika na kutufanya waislamu na wakristo?

Huo ulikuwa ushindi mkubwa  kwa wakoloni,Wazungu na waarabu.

Mamilioni ya WAAFRIKA wakawa sio WAAFRIKA tena.
Wakafanyika watu wanao fanana na waafrika.

WAAFRIKA ambao waliukataa uislamu na ukristo wakaitwa 'wapagani' na kwa hivyo wakadhalauliwa na kuwekwa chini Katika jamii yao wenyewe.

Ndugu zao waliopotea wakazichukia mila na tamaduni zao,na kuziona ni za kizamani,za kishenzi na za kishetani😠.

Watu weusi ndani ya nyumba yao,wakakosa nguvu na kushindwa kupewa nafasi Katika ngazi za ujenzi wa jamii zao.

Na kwasababu ya kuzifuata dini na tamaduni za kigeni, wapumbavu hao wakapewa vyeo na kuitwa waheshimiwa na kuonekana wema Katika jamii yao ya kiafrika iliyopotea ya wapumbavu wenzao  waliokubali kufuata ushenzi wa mzungu na mwarabu.

Na hili  kuharibu kabisa sio tu urithi wetu wa kiafrika lakini pia kuaribu utambulisho wetu wa kiafrika,kisaikolojia, waafrika tukalazimishwa kubadilisha majina yetu na kuchukuwa majina ya Kiarabu na kizungu.

Kuanzia hapo, waafrika waliopotea wakaanza kuwaita watoto wao na kujiita wenyewe Majina ya kitumwa Kama John, Muhammad, Samuel, na Abdullah na wakapewa ukuu katika uwanja wa utawala wa kikoloni, kwa dhana kwamba wao walikiwa wameelimika zaidi kuliko ndugu zao.

Kwaiyo watu weusi nyumbani Afrika na  waliotawanyika ulimwenguni kote mpaka leo wanatembea wamebeba majina ya watumwa na wanyanyasaji wao Wazungu na waarabu,huku tukigeuka vituko mbele ya macho ya watu wa jamii zingine.

Pingu hizi za kisaikolojia bado zimetutia ulemavu waafrika mpaka leo, na kutufanya kuwa wapumbavu na vituko duniani kote.

                        AMKA MWAFRIKA

No comments:

Post a Comment

Pages