IBADA ZA MABABU ZETU
✍🏾Hivi bado unaamini sisi tunao fanya ibada kwa kujiunganisha na Babu zetu tunaabudu mizimu
✍🏾Unaacha kuomba kwa lugha yenu na kutumia majina ya mababu zako kwenye ibada zako unapoteza mda na majina ya mababu wa wenzako. yani Ibrahimu,muhamadi,yesu, na kusema mababu zako ni mizimu😂😂😂
✍🏾KWA taarifa zenu hatuachi KUABUDU asili yetu kupitia tamaduni zetu kwa ibada zilezile zilizo fanywa na Babu zetu munao waita mizimu
“Ndipo tukamlilia BWANA, Mungu wa baba zetu, na kutusikia, akaona mateso yetu, na taabu zetu. ( Kumbukumbu la Torati 26:7 )
".... Wana wa Israeli, (watu wa Afrika) msipigane na BWANA, Mungu wa babu zenu! Hamwezi kushinda!" ( 2 Mambo ya Nyakati 13:12 )
“Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zetu, uwasamehe kwa wema wako wale wanaokuabudu kwa moyo wao wote, ingawa wao si safi. ( 2 Mambo ya Nyakati 12:19 )
“Ezra akasema, Msifuni BWANA, Mungu wa baba zetu! …” (Ezra 7:27).
“Basi, ungameni dhambi zenu kwa BWANA, Mungu wa baba zenu, na kufanya yale yanayompendeza…” (Ezra 10:11).
"Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona Mtumishi wake mwenye haki, na kumsikia akisema kwa sauti yake mwenyewe." ( Matendo 22:14 )
"Mimi ninamwabudu Mungu wa babu zetu kwa kufuata ile Njia ambayo wanasema si ya kweli. Lakini pia ninaamini yote yaliyoandikwa katika Sheria ya Mose na vitabu vya manabii." ( Matendo 24:14 )
✍🏾Yule mungu Alie wapatia Babu zetu mvua,mazao,uzazi,kinga, ndio huyo huyo sisi tutamuabudu na si mwingine ni asili na tuna mshukuru kwa kutujibu maombi yetu ni mwendo wa vibiyu tu
Ninakusifu na kukuheshimu, Mungu wa babu zangu. Umenipa hekima na nguvu; umejibu maombi yangu na kunionyesha - (mimi) yale ya kumwambia mfalme." ( Danieli 2:23 )
MABABU WAWE NANYI 🙏
No comments:
Post a Comment