Breaking

Wednesday, September 28, 2022

MNAMO MWAKA 1963 VIONGOZI WA AFRIKA WALIKUTANA ADDIS ABABA ETHIOPIA


Unajua kwamba idea ya Pan Africanism ilijadiliwa Sana na viongozi wa Afrika Mara nyingi Ila ikishindikana

Mnamo mwaka 1963 viongozi wa Afrika walikutana Addis Ababa Ethiopia kujadili kuhusu kuungana kwa Afrika na utaifa mmoja, walikutana viongozi wa nchi 32 za Afrika wakagawanyika kwenye makundi mawili kikundi cha Kasablanka na kikundi cha Monrovia.
Kikundi cha Kasablanka kilikua kinasema "Afrika Ni kwa ajili ya waafrika walipo nyumbani na waliopo nje ya Afrika na Afrika iungane Sasa" nchi zilizokua upande wa Kasablanka Ni Ghana,Guinea,Mali, Algeria, Egypt, Morroco,Libya kikiongozwa na Kwame Nkrumah

Upande wa Monrovia kulikua na nchi kadhaa Kama Tanzania,Liberia,Nigeria,Congo,Togo n.k huku wakiongozwa na mwalimu Nyerere kikundi cha Monrovia kiliamini muungano wa Afrika usiwe haraka haraka hivyo twende taratibu kwa kuungana kiupandeupande Kama upande wa mashariki ya Afrika(East African community/SADEC) ,upande wa kaskazini wa Afrika(AMU) ,upande wa magharibi (ECOWAS) Kisha tunakuja kuungan wote kwa pamoja sadly Hakuna progress yoyote iliyoonekana mpaka leo miaka 60 bado hatujaungana Tatizo liko wapi?

No comments:

Post a Comment

Pages