Breaking

Wednesday, September 28, 2022

MUAFRIKA RUDI KATIKA ASILI YAKO


Unauliza kivipi dini za wakoloni ni utumwa wa akili kwa Waafrika na Zina athari kwetu dini si dini tu kila mtu na Imani yake? Ngoja nikujibu

1. Dini za kikoloni zinatushawishi kua sisi waafrika ni wafataji tu hatukua na mchango wowote na hatuna mchango wowote.Ukisoma Uislamu kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa Uislamu Ni kuhusu waarabu na mambo yote yanawahusu wåårabu tu
(A) ukitaka kuzungumza na mungu kwenye swala/ maombi Ni lazima ujue lugha ya watu wengine ni lazima uzungumze nae kwa lugha ya wåårabu Ina maana mungu anaelewa lugha moja tu ya kiarabu kwanini nisizungume lugha yangu tu?
(B) waislamu wanaambiwa peponi wote watazungumza kiarabu fasaha ndio Kama lugha rasmi ya peponi na ya kuwajumuisha watu wote kule
(C) mitume yote ya kiarabu na makabila ya huko kwao hakuna mtume alietumwa hata kwa bahati mbaya huku kwetu hata mmoja
(D) sehemu takatifu zote ziko uarabuni na nchi zenye waarabu Makka,Madina na Palestine na ili usamehewe dhambi zako zote Ni lazima uende Makka Kama una uwezo Ni ndoto ya kila muafrika muislamu kwenda hapo
(E) mavazi mataktifu ya Uislamu Ni mavazi ya wåårabu(kanzu,hijabu) waarabu wameanza kuvaa kanzu kabla ya Uislamu kanzu sio vazi la Uislamu
🔑 NIAMBIE wewe sasa waislamu watawaonaje waarabu kama kila kitu wanachotamani kwenye maisha Yao Ni cha wåårabu mtu unazungumza lugha yao, una ndot ya Kwenda kwenye pepo yao, sehemu takatifu yako Ni ya kwao, mavazi yako mataktifu Ni ya kwao, si utawaona Kama wao wamebarikiwa kushinda wew na wao Ni kizazi pendwa cha mungu hii inamadhara makubwa sana kwenye saikolojia ya mwanadamu ndio Mana leo ukiwasema waarabu waislamu wanakuja juu hawataki watu waliochaguliwa na mungu wasemwe vibaya wako radhi kupigana kwa akili Yao watakutukana kwenye comment kisa umewasema waarabu na huu ndio utumwa wa akili tunaouzungumzia kuna watu mapaka wanatamini wafute historia ya wakoloni wao ili tu waonekane wameletewa dini kistaarabu Ila Hakuna dini iliyokuja kistaabu dini zote zimekuja kwa utumwa na maovu jinsi mnavyozidi kua wåårabu ndivyo jinsi mnapoteza uafrika wenu Ile roho ya kiafrika mnapoteza mnajichukia wenyew

2. Dini zinatufundisha tukitaka kukubalika kwa mungu kwanza tujikatae sisi wenyew Yani uache desturi zako zote na uanze kufata desturi za watu wengine ili mungu akupokee unadhani ni huyo mungu Ni wakwako kweli ?

3. Dini zilitumika kututenganisha waafrika na mpaka leo Ni tabu Sana nchi za kiafrika dini zimekua tatizo na udini hautoisha Kama hatutoondoa dini zao

4. Ukienda kwa wakristo pia hivyo hivyo kila kitu Chao kinahusiana na wazungu wa Israel wanaamini wale wamebarikiwa na wao walilaaniwa kwakua Ni kizazi cha mtoto wa Noah alieuona utupu wa babaake hivi inataka kuniambia watu wasijichukie tu Kama ndio wanaaminishwa hivi? Ukiwasema wazungu Leo utawaona wakristo wanakujia juu Ila mbona hao wåzungu hawana mda na nyie hata mkiuliwa ? Mfano mzuri wazungu wanaandamana kwa ajili ya Vita ya Ukraine ila hawajawahi na hawatowahi kuandamana kwaajili ya maafa yanayotokea Afrika hata siku moja ni wewe tu unaumia kwa ajili ya mabwana wako

Rudi kwenye asili yako muafrika achana na dini zao walizotumia kututawala bado zinakutawala kifikra

No comments:

Post a Comment

Pages