Breaking

Wednesday, September 28, 2022

UPANDE WA PILI WA SARAFU 2




2. Anaitwa Mobutu Sese seko kuku Ngbendu wa zabanga alikuwa Raisi wa awamu ya pili nchini Kongo baada ya kufanya mapinduzi mwaka 1965 na kumpindua aliyekuwa raisi wa kwanza wa Kongo Joseph kasavubu.

Katika utawala wake wa miaka 32 nchini Kongo aliweza kufanya mabadiliko mbalimbali Nchini humo Moja ya mabadiliko Muhimu yalifanyika mwaka 1970 ambapo kwa mara ya kwanza nchini Kongo aliianzisha sera iliyofahamika kama "Authenticity policy"kwa maana ya National identity.

Sera hii ya Authenticity ilikusudia kuirudisha Kongo kufuata Tamaduni zao kwa kuacha kufuata Tamaduni za magharibi ambazo zilikiwa zimepamba moto miaka hiyo. Moja ya vitu vilivyofanyika CHINI ya sera ya Authenticity ni pamoja na ;

1. Alipiga marufuku Muziki kutoka magharibi kusikika Kongo badala yake nyimbo za Asili zilipewa kipao mbele.

2. Alipiga marufuku mavazi ya kimagharibi mfano Croptop, high hills,na MATUMIZI ya vipodozi kutoka magharibi.

3.Alipiga marufuku majina yote ya kikristu nchini Kongo badala yake majina ya Asili yalitakiwa kupewa watoto pindi watakopozaliwa kwa mfano majina kama John, Joseph, marry yalipigwa marufuku kabisa. Kusisitiza suala Hilo alianza kubadilisha jina lake yeye mwenyewe kutoka kuitwa Joseph Dêsire Mobutu Mpaka kujiita Mobutu Sese seko kuku Ngbendu wa zabanga.

4.Alibadilisha jina la nchi kutoka Kongo Mpaka Zaire na Mto Kongo ukaitwa Mto Zaire.

5. Alishusha Sanamu zote zilizokuwa za watawala wa Belgium na kupandisha masanamu ya mashujaa wa Africa mfano Patrice Emery Lumumba. N.k

Huyo ndo Mobutu Sese seko kuku Ngbendu wa zabanga.

No comments:

Post a Comment

Pages