Breaking

Wednesday, September 28, 2022

UPANDE WA PILI WA SARAFU 1

UPANDE WA PILI WA SARAFU. 


1. General, Dr. Al_hajji, Field Marshall Iddy Amin Dada wa Uganda. 

 January 25,1971 Baada ya kufanya mapinduzi na kuichukua Nchi mikononi mwa aliyekuwa rais wa Uganda Dr. Milton Obote Iddy Amini aliwafukuza raia wenye asili ya bara la Asia hususani wahindi na sababu kubwa iliyofanya kuwaondoa watu hao nchini Uganda ni pamoja na Unyonyaji uliokithiri. 

Wahindi walitawala shughuli zote za kiuchumi kwa asilimia 97.5% nchini Uganda walijipatia fedha nyingi na hawakuwekeza nchini Uganda fedha zote waliwekeza nchini kwao hususani india na Pakistan hii ilipelekea uchumi wa Uganda kushuka kwa Kasi kutoka 21.3% Hadi 13.6%. 

Wahindi waliitumia Uganda kama sehemu ya kujikusanyia utajiri na kuwekeza kwenye nchi zao na sio kwa manufaa ya Waganda hivyo kufanya nchi kuwa maskini wakati wao wakinufaika.

Wahindi wenye taaluma kama vile  waalimu, madaktari, wanasheria, wataalam wa meno, wakemia, mafundi wa magari walilipwa mshahara usiopungua dollar $1,493 wakati huo Waganda wenye taaluma karibu sawa na hizo walilipwa $243. 

Benki ziliendelea kutoa mikopo kwa wageni na wageni waliitumia mikopo hiyo kuwekeza katika nchi zao. Wahindi walifanikiwa kuwekeza nchini Uingereza kiasi Cha Dollar $725 million kutoka Afrika mashariki pekee. 

Field Marshall Iddy Amin Dada akaamua kuwafukuza raia wote wa kigeni kutoka bara la Asia na kutaka shughuli zote za kiuchumi ziendeshwe na Waganda wenyewe kitendo hicho kilitafsiriwa kama ni ubaguzi na nchi za magharibi hususani Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Pages