Breaking

Wednesday, September 28, 2022

UTUMWA NI NINI?




Utumwa Ni Hali ya mwanadamu kutokua huru kufanya kitu kwa maamuzi yake,kutokua huru kufanya kitu kwa mtazamo wake,kua na msukumo fulani kwenye utendaji wa Mambo bila malipo yoyote

Utumwa uko wa aina mbili (a) utumwa wa kimwili (b) utumwa wa akili/fikra

(A) Utumwa wa kimwili kila mtu anaujua unafungwa mahala fulani au kwa kitu fulani Kisha unatumikishwa kwa lazima bila malipo

(B) utumwa wa akili ndio utumwa mpana sana utumwa huu Ni kwamba akili yako inakua haiko huru kuwaza na kutenda mambo kwa fikra zake Ni lazima update msukumo wa my fulani au mawazo fulani kutenda mambo utumwa huu ndio utumwa mbaya zaidi ya ule wa kimwili utumwa huu unatengemezwa tangu utotoni tunakua nao ndio Mana Ni mbaya zaidi na ndio mgumu kuepuka na kuukataa,

Utumwa huu wa akili ndio utumwa uliopo sasa kwa idadi kubwa Mana ule wa mwili umeshaisha na unasapotiwa na vitu Kama vifuatavyo
1.Elimu na mifumo yake
2.Vyombo vya habari
3. Dini

1. Elimu na mifumo yake ipo kwaajili ya kutengeneza watumwa sio wasomi tunaaminishwa Ni lazima tusome Kisha tupewe ajira na serikali ndo maisha yetu yawe mazuri kwani nani aliesema maisha mazuri Ni lazima utapate shule? Shule hazitufunzi kujiajiri Wala kuwekeza zinatutaka tumalize tutegemee mifumo toka serikalini ndio mana wanafunzi wengi wakimaliza vyuo wanakaa nyumbani kungoja kazi wameshaaminishwa ndio njia Yao pekee ya kufikia lengo la maisha wameshafanya watumwa. Kwenye miaka ya 1910—20 Kama sijakosea serikali ya America na mifumo Yao ya ubepari baada ya kuona inapoteza pesa nyingi kuwalipa wafanyakazi na haina wafanyakazi wengi serikalini ikaamua kutengeneza mfumo wa elimu ambao utawafanya watu watumwa watu warundikane mashuleni wasomi wawr wengi na waajiriwa wawe wachache ili wawalipe mshahara mdogo waajiriwa waliopo kazini Mana kila mtu anaitaka nafasi yako huwezi fanya lolote na huu mfuno ndio mifumo inayotumika hata huku kwetu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa Leo ukisikia mtu fulani tajiri wa kwanza Tanzania au duniani akili yako haiwazi kua itakua Ni daktari au mwalimu akili yako unawaza lazima atakua mfaya biashara,anauza vitu haramu,ana hisa za mabenki na Mambo Kama hayo kwanini unapotaka kua na pesa unawaza kwenda shule? Ni Aina ya utumwa hii tumetengenezwa tayari

(B) Vyombo vyao vya habari: vyombo vyao vya habari vinakutaka uwaze wanavyotaka wao ufanye wanalotaka wao na usifanye wasichokitaka wao wanakupangia Ni mtu gani umepende Nani umchukie nani awe adui yako na Nani asiwe wanaotupa habari wanatupa upande ambao wao wanapenda wewe ujue sio upande ambao Ni sahihi mzuri leo ukimuuliza mtu kwanini unamchukia Putin? Atakuambia kwasababu anaua watu wasio na hatia mtu huyo huyo ukimuuliza unamchukia Obama atakujibu hapana kana kwamba Obama hakuua watu Ni vyombo vyao tayari vimeshampa adui yao awe wake CNN,BBC, Aljazeera zote ziko kimaslahi sio kwa taarifa ingekua kwa taarifa zingekua zinatoa taarifa za Mambo wanayoyafanya wazùngu Afrika na wachina wanayoyafanya Congo kwanini hawasemi Kuna watu wapo nyuma ya hayo Mambo na wao ndio wanaomiliki hivyo vyombo vya habari itakua Ni ujinga kuwaamini kila wanachosema tuchukue mfano mzuri wa hapa Afrika Muammar Gaddafi aliuwawa na watu wake mwenyewe kwasababu walikua watumwa wa fikra za vyombo vya habari walishaaminishwa kua Gaddafi Ni dikteta ila Ila mbona hivyo vyombo havisemi marekani Ni serikali ya kidikteta inazilazimisha nchi za Afrika kutofanya biashara na Urusi huu sio udikteta? Mbona hawaongelei Mambo wanayofaya Afrika nanchi za kiarabu(mashariki ya Kati) Ila wanaongelea tu ya wenziowao wanataka uwe mtumwa wao uwazw wanachokitaka amka kifikra Sasa escape the Matrix

No comments:

Post a Comment

Pages