Breaking

Wednesday, September 28, 2022

AFRIKA INAVITUO VYA KIJESHI


Afrika Ina vituo vya kijeshi(military bases) vingi zaidi vya nchi za mgharibi na Asia kuliko bara lolote hapa ulimwenguni na vituo vinazidi kuongezeka siku kwa siku 

Hivi vituo vinajengewa kwenye zile sehemu zenye malighafi ili waibe vizuri na kwa urahisi Kama kweye madini,mafuta,maziwa n.k Ufaransa imeweka vituo vyake vyote pembezoni mwa migodi ya Uranium,Cobalt n.k Marekani na Chin apia

Kama ulikua hujui kwasasa Kuna Vita bardi ya wachina na wamarekani juu ya malighafi za Afrika kila mmoja anataka awe na ushawishi mkubwa zaidi kwenye malighafi zetu mfano mzuri Ni Dijiibout 🇩🇯 nchi ambayo mchin na mmarekani wanakuza kambi zao za jeshi tu kila siku mpaka wanakaribiana kiasi cha mita 500 tu ukienda Congo kitu hicho hicho wanakuza wigo wa kambi zao kila siku na mvutano Ni mkubwa wa rasilimali za watu weusi ambao wamelalal usingizi mzito

Utofauti wa mmarekani na mchina Ni kwamba mchina anakuja Afrika kwa vigezo vyao madeni na ushawishi wa kibiashara za kihuni na za mitego Ila mmarekani Yuko radhi kutengeneza vita, magonjwa,machafuko,njaa ili tu afike anapopataka akishafanya hivyo anajua atawala tu Kisha atajenga vituo vya kijeshi atakavyo na ana uwezo wa kuwavamia muda wowote mkijaribu kuleta pingamizi ngumu

Afrika jitambue hakuna wa kukusaidia jisaidie mwenyewe usidhani Wala kutegemea aliekutengenezea tatizo aje kukusaidia huo Ni uongo ulioko wazi

No comments:

Post a Comment

Pages