Breaking

Wednesday, September 28, 2022

MTU MWEUSI ALIZALILISHWA NA WAZUNGU


Anaitwa George McLaurin mtu mweusi wa kwanza kuandikishwa katika Chuo Kikuu cha Oklahoma mwaka 1948, alilazimishwa kuketi kwenye kona mbali na wazungu.
Lakini jina lake limesalia kwenye orodha ya heshima kama mmoja wa wanafunzi watatu bora chuoni.
Haya ni maneno yake:
''Baadhi ya wanachuo wenzangu walinitazama kama mnyama, hakuna aliyezungumza nami, kwa walimu ni kama sikuwepo, walijibu maswali yangu mara chache. Nilijituma sana, hadi wenzangu kuanza kunitafuta na walimu walianza kunitilia maanani. Nilianza kua wa maana kwao."
Elimu ina nguvu kuliko silaha.

No comments:

Post a Comment

Pages