Breaking

Wednesday, September 28, 2022

UNAJUA KWANINI HAUSOMI UCHUMI SHULENI KWA LUGHA YAKO?


Unajua Ni kwanini hausomi uchumi shuleni kwa lugha yako? Na sio uchumi tu masomo yote?

Hi kwasababu haumiliki uchumi wako uchumi wako wanaumiliki watu wengine ukienda China wanasoma masomo yote kwa lugha yao ya kichina,ukienda Ufaransa wanasoma kwa lugha yao ya kifaransa,ukienda German wanasoma uchumi kwa lugha yao ya kijerumani, ukienda Australia na marekani wanasoma uchumi kwa lugha yao kingereza ukienda Japan,Korea na kote huko Ila ukija Afrika tunasoma kwa lugha za watu eidha lugha ya wåzungu, lugha ya wafaransa lugha ya wareno na kadhalika Isipokua lugha zetu Ni kwasababu hatumiliki uchumi wetu tunaosoma kwa lugha zao ndio wanaomiliki uchumi wetu watu kote dunaiji wako bussy kuandika na kutafsiri vitabu kwenda kwenye lugha zao sisi tuko busy kutetea shule ziongeze na zikazie ufundishaji wa kingereza mashuleni tuko busy kubishana kati ya wakenya na Watanzania Nani wanazungumza kingereza vizuri tunabishana Nani mtumwa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages